Click here to view Mama Ye! Tanzania in English

Mwanzo > Mac > Tusiuvumilie ukeketaji Tanzania

Tusiuvumilie ukeketaji Tanzania

Nchini Tanzania makundi mengi yamefanya kampeni nab ado yanaendelea kufanya kampeni dhidi ya Ukeketaji. Kwa mfano, Mlimbwende wa Tanzania (Miss Tanzania 2016/17) Diana Edward yeye anajihisi ana deni ajiunge na kampeni kwani kwani anahisi amenusurika kukeketwa alipoishi Umasaini utotoni mwake, jamii ambayo inathamini sana mila hii.

Vitendo hivi vyenye madhara makubwa kutokomezwa kwake kumekuwa jambo gumu. Mafanikio yaliyofikiwa kwa miaka mingi ya kueliisha jamii dhidi ya ukeketaji, kuwajengea ujasiri wasichana kukataa na kuwashawishi  viongozi wa kimila kuikomesha mila hiyo hayajaleta matokea ambayo wanaharakati wanatamani wayafikie.

Takwimu zinaonnyesha kupungua kwa ukeketaji lakini kwenye baadhi ya mikoa tatizo bado ni kubwa sana

Kwenye ukurasa wake wa Facebook, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu (MB)  anakiri kuwa , “ Ukeketaji bado ni tatizo nchini”. Kwa mujibu wa takwimu za hivi karibuni za Utafiti wa Demografia na Afya 2015, 10% ya wanawake wa Tanzania wamekeketwa huku mikoa inayoongoza kwa matukio hayo ikiwa ni Manyara (58%), Dodoma (47%) na Arusha (41%).

Namba hizi zinatisha! Lakini matumaini yapo pia kwani inaripotiwa ya kuwa, wakati  “mwanammke mmoja kati ya kila wanawake kumi Tanzania amekeketwa, uelewa kuhusiana na ukeketaji unaongezeka kadiri kiwango cha elimu kinavyoongezeka, kuanzia 71% kwa wanawake wasio na elimu hadi kufikia 97% kwa wanawake wenye elimu ya sekondari au zaidi.” Jambo la kusisimua zaidi ni kuwa wanawake wapatao 95% wanaamini kuwa ukeketaji haukubaliki kidini na pia utaratibu huu unapaswa kuachwa.

Miss Tanzania, akiunga ongeza nguvu kwenye kasi ya wanaharakati wengine, amezindua  kampeni yake iitwayo Dondosha Wembe ambapo anafanya kazi na jamii za Wamaasai, akitumia uzoefu na ukaribu wake na jamii hizo na mila zao, Diana nae anajitahidi kuutokomeza ukeketaji.

Miss Tanzania 2016/17 Diana Edward alipokuwa na mahojiano na Ayo TV

 “Mimi ni mmoja wao kwa hiyo ni rahisi kuniamini,” amesema katika mahojiano yake na shirika la BBC “Nikiwa huko Umasaini navaa kama wao na kushiriki shughuli zao za kila siku.”When I am out there I dress just like them and participate in their daily activities.”

Serikali inaunga mkono jitihada kama hizo. Waziri Ummy Mwalimu anasema “jambo hili halikubaliki. Tushiriki Kutokomeza Ukeketaji Nchini. Inawezekana kutokomeza kabisa Ukeketaji nchini hata kabla ya 2030 endapo kila mmojawetu atashiriki vita hii. Kwa Pamoja Tunaweza. #EndFGM

 

Chukua hatua sasa....Pata taarifa nyingine kuhusu ukeketaji ulimwenguni kupitia tovuti ya Girl Generation Campaign

Rudi juu