Click here to view Mama Ye! Tanzania in English

Mwanzo > Mac > Kuziba pengo kwa kutumia wahudumu wa afya kwenye jamii

Kuziba pengo kwa kutumia wahudumu wa afya kwenye jamii

Ulimwenguni kuna uhaba wa wahudumu wa afya milioni 7.2 – na idadi hii inatarajiwa kuongezeka hadi kufikia milioni 12.9 ifikapo mwaka 2035. Wahudumu wa afya ywa jamii (CHWs) ni mbadala endelevu na wenye ufanisi katika kuziba pengo la uhaba  huo na wanaweza kufikisha huduma hadi maeneo ya mbali na magumu kufikika  kwenye nchi zinazoendelea. 

CHWs wanaweza kutoa mchango mkubwa katika kuchunguza na kutoa tiba kwa magonjwa ya kawaida ya kuambukiza na ya watoto, wanaweza kutoa huduma kwa wajawazito na watoto wachanga, na kuelimisha jamii kuhusu hatua za mbali mbali za kinga kiafya.  Wanaweza pia kutoa rufaa kwa wagonjwa waende hospitali  pale ambapo tiba ya kitaalamu zaidi inahitajika.

Jopo la Wataalamu wa Malaria limekuwa likifanya kazi Afrika nzima kupanua wigo wa kazi za wahudumu wa afya wa jamii ili kusogeza huduma za afya karibu na wanajamii ambao wanazihitaji zaidi. Mradi wetu unashughulika kutafuta mbinu mbali mbali kuboresha ufanisi wa huduma za kada hii, ikiwa ni pamoja na kupitia teknolojia ya simu za kiganjani na majadiliano katika jamii.

 Kibonzo hiki kinaonyesha jinsi CHWs kama Laurinda anavyoboresha huduma ya afya katika jamii zao, anachohitaji ni ili kumsaidia kufanya kazi yake na nafasi ya viongozi na watoa maamuzi katika kuziba pengo la uhaba wa wahudumu wa afya. .

Ili kuangalia kibonso, bofya hapa>

Document type 
Rudi juu