Click here to view Mama Ye! Tanzania in English

Mwanzo > Nyenzo > Je, u mjamzito?

Je, u mjamzito?

Kwenye ukurasa huu kuna namba za simu, anuani za tovuti na nyenzo kadhaa zitakazoweza kukusaidia katika kipindi chako cha ujauzito
12th Feb 2013

Wazazi Nipendeni

Wazazi Nipendeni inatafsiri kwa vitendo CARMMA kwa kuwawezesha wajawazito na wenzi wao kuchukua hatua muhimu ili ujauzito uwe wa afya na uzazi uwe salama. 

12th Feb 2013

Chezasalama

Tovuti ya Chezasalama inaendeshwa na Femina HIP na ina taarifa muhimu kwa afya ya uzazi kwa ajili ya vijana. Fuata kipengele cha 'mapenzi' kuna taarifa mbali mbali kuhusiana na ujauzito. 

11th Feb 2013

Orodha ya Hospitali Duniani - Tanzania

Chanzo hiki cha taarifa mtandaoni kimeorodhesha hospitali nyingi duniani kote. Ukurasa huu unakupeleka kwenye orodha ya Tanzania ambako utaona hospitali za kawaida na zile maalum.

11th Feb 2013

Orodha ya Huduma za Afya

Orodha hii ina idadi kubwa ya vituo vya afya nchini, kuanzia hospitali hadi kliniki za kujifungulia na makampuni ya bima za afya yamo humo. Tafuta eneo unaloishi, au mji na kitongoji upate taarifa zaidi.  

11th Feb 2013

Hospitali ya Aga Khan Dar es Salaam

Hospitali ya Aga Khan jijini Dar es Salaam ina moja ya vitengo vyenye huduma bora za uzazi nchini. Wana utaalamu wa uangalizi wa watoto, wanawake, ambapo pia hutoa huduma ya upimaji kansa ya titi na ya kizazi.  

05th Feb 2013

Kipeperushi cha CARMMA kuhusu 'Umuhimu wa chanjo'

Je mwanangu anahitaji chanjo? Kipeperushi hiki kutoka CARMMA kinakupa sababu nzuri kabisa kujua ni kwa nini Mama na Mwana wanahitaji chanjo na kinga ipatikanayo kutokana na chanjo--Kumbuka chanjo ni bure! 

28th Jan 2013

Hatua za ujauzito

Ujauzito wa kawaida huchukua takriban wiki 40. Wiki hizo hugawanywa katika hatua tatu ziitwazo kwa lugha ya Kiingereza 'trimesters.' Jifunze zaidi kuhusi kila hatua kwa kusoma makala hii iliyochapishwa na Women's Health.

24th Jan 2013

Alama saba za hatari katika ujauzito

Ujauzito unakuja kwa namna tofauti tofauti kwa watu mbali mbali. Kuna dalili zinazoweza kusubiria tarehe yako inayofuata kwenda kliniki lakini nyingine zinahitaji huduma ya haraka. Soma makala hii iliyoandikwa na Denise Mann kujua tofauti.